Mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa BURKINA FASO atangazwa kuwa kiongozi mpya
Mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa BURKINA FASO BLAISE COMPAORE ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo baada ya walinzi wa rais wa mpito wa nchi hiyo
Jenerali GILBERT DIENDERE

Mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa BURKINA FASO BLAISE COMPAORE ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo baada ya  walinzi wa rais wa mpito wa nchi hiyo kupindua serikali.

Taarifa iliyotolewa na walinzi hao imesema Jenerali GILBERT DIENDERE, aliyekuwa mkuu wa majeshi chini ya Rais wa zamani BLAISE Compaore, ndiye aliyepindua serikali ya kaimu Rais Michel Kafando

Walinzi hao wanadaiwa kufyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana OUAGADOUGOU kupinga hatua ya wanajeshi hao kupindua nchi.

Rais FRANCOIS HOLLANDE wa UFARANSA ameshutumu hatua ya walinzi hao wa rais ya kupindua serikali.ametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Kaimu Rais MICHEL KAFANDO na Waziri Mkuu ISAAC ZIDA.

Serikali ya BLAISE COMPAORE aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 27 iliondolewa baada ya maandamano ya raia mwaka jana na kuundwa serikali ya  ya mpito ilitarajiwa kukabidhi mamlaka kwa serikali ambayo ingechaguliwa kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 11

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI