Rais OBAMA amualika Ikulu mvulana aliyetengeneza saa
Rais BARRACK OBAMA amemualika ikulu mvulana wa kiislamu mwenye umri wa miaka 14 mara baada ya kushikiliwa na polisi kwa muda baada ya kupeleka shuleni saa aliyoitengeneza mwenyewe
AHMED MOHAMED

Rais BARRACK OBAMA amemualika ikulu mvulana wa kiislamu mwenye umri wa miaka 14 mara baada ya kushikiliwa na polisi kwa muda baada ya kupeleka shuleni saa aliyoitengeneza mwenyewe nyumbani na mwalimu wake kudhania kuwa ni bomu.

Kupitia ukurasa wa TWITTER Rais OBAMA amemsifu AHMED MOHAMED kwa saa yake hiyo na kuwataka watoto wengine kuhamasika na kufurahia sayansi kama AHMED.

Siku ya jumatatu kijana huyo alishikiliwa na polisi baada ya mwalimu wake kutoa taarifa polisi kuhusu chombo alichokuja nacho shuleni mwanafunzi huyo.

kikundi cha kiislamu nchini Marekani kilizungumzia suala hilo kuwa kijana huyo alikamatwa kwa kuwa ana Imani ya Kiislamu.

Taarifa ya kukamatwa kwake ilileta hisia tofauti katika mitandao ya kijamii.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI