Viwavijeshi waharibu mazao Bagamoyo
Wadudu aina ya viwavijeshi wamevamia wilaya ya BAGAMOYO na kuharibu Zaidi ya ekari 20 za mazao yaliolimwa katika kata za YOMBO na KIBINDU.
Kiwavi Jeshi

Wadudu aina ya viwavijeshi wamevamia wilaya ya BAGAMOYO na kuharibu  Zaidi ya ekari 20 za mazao yaliolimwa  katika kata za YOMBO na KIBINDU.

 

Mazao yaliyoharibiwa kwa kiasi kikubwa ni mpunga na mahindi jambo linalowafanya wananchi wa eneo hilo kuhofia kukumbwa na uhaba wa chakula.

 

Mkuu wa wilaya ya BAGAMOYO Alhaji MAJID MWANGA amekiri  wilaya yake kuvamiwa na viwavi jeshi huku akibainisha maeneo yalioathiriwa zaidi kuwa ni kata ya KIBINDU na Yombo

 

Akizungumzia tatizo hilo mkuu wa mkoa wa PWANI EVARISTI NDIKILO amemuagiza afisa kilimo wa wilaya aya BAGAMOYO kupeleka haraka dawa iliyobaki kwa ajili ya kupulizia katika maeneo yalioathirika zaidi.

 

 

JOSEPH CHEWALE

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI