Wachezaji wengi zaidi kushiriki Junior NBA
Jumla ya wachezaji 900 wa mchezo wa kikapu wenye umri wa chini ya miaka 14 wanashiriki mashindano ya Junior NBA kwa mwaka huu.
Baadhi ya Manahodha wa timu zilizoshiriki mashindano ya Junior NBA miaka ya nyuma.

Jumla ya wachezaji 900 wa mchezo wa kikapu wenye umri wa chini ya miaka 14 wanashiriki mashindano ya Junior NBA kwa mwaka huu.

 

Mratibu wa mashindano hayo Bahati Mgunda ameiambia TBC kuwa ongezeko hilo limekuja kutokana na kuanzishwa kwa mashindano ya wasichana tofauti na mwaka uliopita uliokuwa na mashindano ya wavulana pekee

 

Mashindano hayo yanafanyika kwa mwaka wa pili sasa  yakiwa na lengo la kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi wa mchezo  wa kikapu lengo ambalo limeanza kuonyesha mwanga wa mafanikio.

 

 

JANE JOHN

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI