Wafanyabiashara washauri kuepuka bidhaa zinazofanana
Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara JOHNSON MINJA amewashauri wafanyabiashara kununua bidhaa kutoka nchi mbalimbali ili kuepuka kuingiza nchini bidhaa zinazofanana.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara, JOHNSON MINJA.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara JOHNSON MINJA amewashauri wafanyabiashara kununua bidhaa kutoka  nchi mbalimbali ili kuepuka kuingiza nchini bidhaa zinazofanana.

Akizungumza na wawakilishi wa kampuni kumi kutoka  nchini MAURITIUS waliokuja kuangalia fursa za kibiashara nchini MINJA amesema bidhaa zinazouzwa katika maeneo mbalimbali zinafanana kutokana na bidhaa hizo kutoka katika nchi moja jambo ambalo halitakiwi.

Kwa upande wake afisa biashara za nje kutoka  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara  nchini TANTRADE STEVEN KOBELO amesema bidhaa ambazo watanzania wanaweza kupeleka MAURITIUS ni vyakula pamoja na malighali ya kutengenezea nguo. 

VUMILIA MWASHA

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI