Rais JOHN MAGUFULI amewataka wananchi kujikita katika shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao
Rais JOHN MAGUFULI amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kuhakikisha wanajikita katika shughuli zitakazoliwezesha taifa kupata maendeleo
Rais MAGUFULI akihutubia muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara eneo la Ubungo leo tarehe 20/03/2017.

Rais  JOHN MAGUFULI amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kuhakikisha wanajikita katika shughuli zitakazoliwezesha taifa kupata  maendeleo na kuachana na tabia ya kutumia mitandao katika shughuli zisizokuwa na maana.

 

Rais MAGUFULI amesema hayo jijin DSM muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara eneo la Ubungo huku akimtaka mkuu wa mkoa wa DSM PAUL MAKONDA kufanya kazi bila kujali maneno wanayosambaa katika  mitandao ya kijamii.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI