Waziri Mkuu Majaliwa awakaribisha wawekezaji wa Iran
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini IRAN kuja kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo na uvuvi.
Waziri Mkuu, KASSIM MAJALIWA na Balozi wa IRAN hapa nchini, MOUSA FARHANG walipokutana Jijini DSM.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini IRAN kuja kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo na uvuvi.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli alipokutana na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang kwenye makazi yake Oysterbay Jijini DSM.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake hivyo wanahitaji  uwekezaji mkubwa kwenye sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Balozi Farhang  ameipongeza Serikali kwa dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi na kupambana na dawa za kulevya na ufisadi.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI