Wakulima watakiwa kuongeza thamani ya mazao
Mkurugenzi msaidizi wa taarifa za masoko na utafiti kutoka wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji Leo Lyayuka amewashauri wakulima kuongeza thamani mazao ili yaweze kuuzwa kwa bei nzuri sokoni.

Mkurugenzi msaidizi wa taarifa za masoko na utafiti kutoka wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji Leo Lyayuka amewashauri wakulima kuongeza thamani mazao ili yaweze kuuzwa kwa bei nzuri sokoni.

Akizindua matokeo ya utafiti juu ya umuhimu wa uchakataji bidhaa za kilimo uliofanywa na taasisi ya utafiti wa masuala ya uchumi- ESRF- Lyayuka amesema mazao yaliyoongezwa thamani yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu na kuuzwa kwa bei nzuri sokoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt Tausi Kida amesema utafiti huo umebaini kuendelea kuwepo changamoto nyingi kwenye sekta ya kilimo ikiwemo matumizi ya teknolojia duni za kilimo.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI