Mchele washuka bei Tandale
Bei ya mchele katika soko la Tandale jijini DSM imeanza kushuka baada ya wakulima kuanza kuuza mpunga ulioko kwenye maghala ili kutoa nafasi ya kuhifadhi mpunga mpya.
Mchele, Sokoni.

Bei ya mchele katika soko la Tandale jijini DSM imeanza kushuka baada ya wakulima kuanza kuuza mpunga ulioko kwenye maghala ili kutoa nafasi ya kuhifadhi mpunga mpya.

Makamu mwenyekiti wa nafaka katika soko la Tandale John Barua amesema mchele  wa bei ya chini kwa sasa unapatikana kwa shilingi 1600 tofauti na wiki chache zilizopita ambapo bei ya chini ya mchele ilikuwa shilingi 1900.

Kuhusu maharagwe BARUA amesema kuwa upatikanai wake umekuwa hauridhishi kwa sababu kiasi kikubwa cha maharagwe yanayofika sokoni hapo yanakuwa mabichi na mengine yanakuwa yameharibika kwa kunyeshewa na mvua.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI