Ahmad Ahmad, rais mpya wa CAF
Ahmad Ahmad wa Madagascar amechaguwaliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) kwa kupata kura 34 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CAF uliofanyika Adiss Ababa nchini Ethiopia.
Rais mpya wa shirikisho la soka barani Africa (CAF), Ahmad Ahmad wa Madagascar

Ahmad Ahmad wa Madagascar amechaguwali kuwa Rais wa shirikisho la soka  barani Africa (CAF) kwa kupata kura 34 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CAF uliofanyika Adiss Ababa nchini Ethiopia.

 

Aliyekuwa Rais wa sasa wa CAF, Issa Hayatou ambaye ni raia wa Cameroon amebwagwa na mpinzani wake kwa kupata kura 20, Hayatou aliingia madarakani tangu mwaka 1988.

 

Kwa upande wake, Rais wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF , Leodgar Tenga ambaye alikuwa akiwania nafasi ya uwakilishi katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu, kura hazikutosha.

 

 

JANE JOHN

MACHI 16, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI