Waandanamanaji Guantemala wamtaka rais ajiuzulu
Mamia ya waandamanaji katika Mji wa Guatemala City nchini Guatemala wamekwenda hadi katika eneo la Ikulu ya nchi hiyo wakimshinikiza Rais Jimmy Morales wa nchi hiyo kuachia madaraka.
Rais Jimmy Morales wa Guatemala.

Mamia ya waandamanaji katika Mji wa Guatemala City nchini Guatemala wamekwenda hadi katika eneo la Ikulu ya nchi hiyo wakimshinikiza Rais Jimmy Morales wa nchi hiyo kuachia madaraka.

Watu hao wanataka Rais Jimmy Morales awajibike baada ya wasichana 39 kufa kwa moto katika kituo cha kulelea watoto cha San Hosee.

Hasira za watu hao zimeongezeka, baada ya kugundua kuwa wasichana hao walikuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na wakati moto ukiwaka walikuwa wamefungiwa katika darasa moja.

Habari zinasema chanzo cha moto huo ni msichana mmoja aliyeuwasha baada ya kukasirishwa na vitendo vya unyanyasaji ambavyo mabinti hao wamekuwa wakifanyiwa.

GHANIA JUMBE

MACHI 12, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI