Kampuni zatakiwa kujioroshesha kuuza Hisa
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dakta Ashatu Kijaji amezitaka kampuni za mawasiliano 63 ambazo hazijaorodhesha kuuza hisa zao katika soko la hisa la Dsm DSE kuhakikisha wanakamilisha kabla ya muda waliopewa.
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dakta Ashatu Kijaji (katikati), viongozi wa Vodacom na wageni wengine wakizindua uuzwaji wa hisa wa kampuni hiyo.

Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dakta Ashatu Kijaji amezitaka kampuni za mawasiliano 63 ambazo hazijaorodhesha kuuza hisa zao katika soko la hisa la Dsm DSE kuhakikisha wanakamilisha kabla ya muda waliopewa.

Akizungumza wakati wa kuzindua uuzaji wa hisa za Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania Plc Jijini Dsm, Dakta Kijaji amesema kampuni hiyo imekuwa ya kwanza kutekeleza sheria ya eloctroniki na mawasiliano ya posta EPOCA na sheria ya fedha ya mwaka 2016 inayotaka makampuni ya simu kumilikisha asilimia 25 ya hisa zao kwa umma

Kuhusiana na mchakato wa ununuaji wa hisa hizo mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Ian Ferrao amesema wanaohitaji watembelee matawi yote ya benki ya NBC na mawakala wa soko la hisa la DSM DSE waliopo nchi nzima na hisa moja inauzwa kwa shilingi 850

ELIZABETH MRAMBA

MACHI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI