UN yahofia Sudan Kusini kukumbwa na mauaji ya Kimbari
Taarifa mpya ya Umoja wa Mataifa imesema SUDAN KUSINI huenda ikakumbwa na mauaji ya kimbari kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo.
Hali ya usalama katika nchi ya SUDAN KUSINI ni tete.

Taarifa mpya ya Umoja wa Mataifa imesema SUDAN KUSINI huenda ikakumbwa na mauaji ya kimbari kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo.

 

Taarifa hiyo imetolewa ikiwa ni miezei saba  baada ya matokeo ya uchunguzi wa kamisheni ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa SUDAN Kusini kuhusu masuala ya haki za binadamu.

 

Taarifa imesema kumekuwepo na shutuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamu zinazotekelezwa na wanajeshi wa pande zote mbili kwa kufanya vitendo vya mauaji, udhalilishaji wa kijinsia na uporaji.

 

Mpaka sasa watu zaidi ya Milioni Moja na nusu wamekimbia nchini humo na kuelekea katika nchi jirani katika kipindi cha miaka mitatu ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe pamoja na hali ya njaa inayoikabili nchi hiyo.

 

 

MARHTA NGWIRA

MACHI 09, 2017  

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI