Uwanja wa Ndege wa Abuja wafungwa kwa wiki 6
NIGERIA imefunga uwanja wa ndege katika mji wa ABUJA kwa muda wa wiki sita ili kutoa fursa ya matengenezo kufanyika uwanjani hapo.
Uwanja wa Ndege wa Abuja

NIGERIA imefunga uwanja wa ndege katika mji wa ABUJA kwa muda wa wiki sita ili kutoa fursa ya matengenezo kufanyika uwanjani hapo.

       

Kutokana na matengenezo hayo watu watakaokuwa wakisafiri kwenda mjini ABUJA wanashauriwa kwenda katika mji wa KADUNA, Kaskazini mwa nchi hiyo ingawaje baadhi ya mashirika ya ndege hayataki kutumia uwanja huo.

        

Habari zinasema hatua ya kufunga uwanja huo imekuja baada ya baadhi ya mashirika ya ndege kutishia kusitisha safari kutokana na sababu za kiusalama.

 

Njia ya kuruka katika uwanja wa ndege ABUJA inaelezwa kuharibika kwa kiwango ambacho inahitaji matengenezo makubwa.

 

 

DOROTHY MMARI

MACHI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI