Benki ya DCB yasitisha mikopo Manispaa ya Kinondoni
Benki ya kibiashara ya DCB imesema imesitisha kutoa mikopo kwa vikundi vya wakina mama na vijana wajasiriamali wa manispaa ya kinondoni kutokana na kupisha zoezi la mgawanyiko wa manispaa hiyo na Ubungo lililokuwa linaendelea
Mkurugenzi mtendaji wa DCB, EDMUND MKWAWA

Benki ya kibiashara ya DCB imesema imesitisha kutoa mikopo kwa vikundi vya wakina mama na vijana wajasiriamali wa manispaa ya kinondoni kutokana na kupisha zoezi la mgawanyiko wa manispaa hiyo na Ubungo lililokuwa linaendelea.

 

Mkurugenzi mtendaji wa DCB EDMUND MKWAWA amesema  mpaka sasa manispaa hizo hazijasema lolote juu ya kuwakopesha wajasiriamali hao  na wala hazijapeleka fedha kwa ajili ya kuwakopesha vijana na wakina mama toka mwaka jana.

 

kwa upande wake meneja wa mikopo ya vikundi wa DCB  MARIA KABEHO amesema hapo awali benki hiyo ilitoa mkopo kwa vikundi vya wakina mama na vijana wajasiriamali wa manispaa ya kinondoni katika kata 34 ambapo kata 4 zinasumbua kwenye marejesho.

 

 

VUMILIA MWASHA

MACHI 7, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI