Mradi wa MUVI wawawezesha wakulima wajasiriamali
Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini SIDO Prof. Sylvester Michael Mpanduji amesema mradi wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini MUVI umewawezesha wakulima na wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini SIDO, Prof. Sylvester Michael Mpanduji

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini SIDO Prof. Sylvester Michael Mpanduji amesema mradi wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini MUVI umewawezesha wakulima na wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo na kuongeza thamani ya mazao yao.

 

Akizungumza wakati wa  tathmini ya mradi huo jijini DSM  uliofanyika katika mikoa saba kwa miaka tisa Profesa Mpanduji amesema ili mradi huo uendelee kuwanufaisha wajasirimali halmashauri zinatakiwa kuendeleza  miradi midogo midogo  iliyoanzishwa chini ya  mradi huo wa MUVI.

 

Kwa upande wake afisa mwandamizi wa shirika la mfuko wa maendeleo ya kilimo la Umoja wa Mataifa IFAD MWATIMA JUMA ambao ndiyo wafadhili wa mradi huo amesema baada ya mradi wa MUVI kukamilika  hilo linatarajiwa kuanzisha mradi mwingine wa maziwa.

 

 

VUMILIA MWASHA

MACHI 7, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI