BRAZIL waanza maandalizi ya sherehe za kijadi
Serikali ya BRAZIL imewatawanya askari wake wapatao elfu TISA katika mitaa mbalimbali ya mji wa RIO DE JENEIRO, kabla ya taifa hilo kuanza sherehe za kijadi nchini humo, maarufu kama CARNIVAL, zinazofanyika kila mwaka.
Sherehe za kijadi nchini BRAZIL, maarufu kama CARNIVAL

Serikali ya BRAZIL imewatawanya askari wake wapatao elfu TISA katika mitaa mbalimbali ya mji wa RIO DE JENEIRO, kabla ya taifa hilo kuanza sherehe za kijadi nchini humo, maarufu kama CARNIVAL, zinazofanyika kila mwaka.

Sherehe za CANIVAL, ambazo ni maarufu sana katika mji wa RIO DE JENEIRO, zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. Serikali ya BRAZIL imelazimika kupeleka askari kwenye mji huo, kwa vile askari Polisi wengi nchini wako katika mgomo wa kufanya kazi.

Askari hao waligoma kufanya kazi wakidai nyongeza ya mishahara, hali iliyosababisha ghasia kuongezeka katika mji mbalimbali ya nchi hiyo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu MIA MOJA NA THELATHINI.

Licha ya serikali kuamuru askari hao warudi kazini na kuacha mgomo wao, ndugu za askari hao waliendelea na maandamano wakiwatetea askari hao na kusema kuwa hawatasimamisha maandamano hayo hadi hapo haki wa ndugu zao itakapotendeka.

NYAMBONA MASAMBA

FEBRUARI 15, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI