BARRACK na MICHELLE OBAMA wenza wenye mvuto zaidi siku ya wapendanao duniani
Tarehe 14 februari kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wapendanao ambapo kwa mujibu wa mtandao wa YAHOO BARRACK na MICHELLE OBAMA ndio wenza wenye mvuto zaidi katika siku hiyo ya wapendanao
BARRACK na MICHELLE OBAMA

Tarehe 14 februari kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wapendanao ambapo kwa mujibu wa mtandao wa YAHOO BARRACK na MICHELLE OBAMA ndio wenza wenye mvuto zaidi katika siku hiyo ya wapendanao

 

Katika kusherehekea sikukuu ya wapendanao duniani Rais mstaafu wa MAREKANI BARRACK OBAMA na mkewe MICHELLE OBAMA wamekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mara baada ya kutumiana ujumbe wa kutakiana heri ya siku hiyo kupitia kurasa zao za mtandao wa kijamii tweeter.

 

Wanandoa hao waliomaliza muda wao madarakani mwezi januari mwaka huu wapo wakiendela na mapumziko katika kisiwa.

 

Michelle alituma picha ya miguu inayohisiwa kuwa ni yake na ya mume wake Barrck Obama wakiwa wamekaa katika mchanga wa bahari. Obama naye alituma picha yao ya zamani wakati wakiwa bado Ikulu ya Marekani.

 

Wapenzi hao waliofunga ndoa miaka 23 iliyopita wamekuwa watu mashuhuri kwa kuonesha upendo wao hadharani hata kipindi wakiwa madarakani wamekuwa wakichukuliwa kama mfano mzuri wa wenza mashuhuri wanaopendana kwa dhati.

 

 

LEAH MUSHI

FEBRUARI 15, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI