TIFFANY TRUMP atengwa katika maonesho ya wiki ya mitindo
Mtoto wa pili wa kike wa Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI, TIFFANY TRUMP amepata hali ngumu kama dada yake IVANKA TRUMP katika maonesho ya wiki ya mitindo NEW YORK MAREKANI.
TIFFANY TRUMP

Mtoto wa pili wa kike wa Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI, TIFFANY TRUMP amepata hali ngumu kama dada yake IVANKA TRUMP katika maonesho ya wiki ya mitindo NEW YORK MAREKANI.

 

TIFFANY ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho hayo ya PHILIPP PLEIN alijikuta akiwa amekaa pekeyake kwenye mstari wa mbele baada ya wahariri wa habari za mitindo kugoma kukaa karibu yake na kwenda kukaa viti vya nyuma.

 

Wahariri hao walituma picha katika ukurasa wa kijamii wa Tweeter zikionesha mtoto huyo wa rais akiwa amekaa pekeyake huku viti vya pembeni yake vikiwa havina watu.

 

Siku ya pili ya kuhudhuria maonesho hayo TIFFANY alisikika tena kwenye vyombo vya habari mara baada ya mwanamuziki MADONNA kuchelewa saa moja kwenye maonesho hayo ili asikutane na binti huyo.

 

MADONNA amekuwa akikosoa utawala wa Rais DONALD TRUMP na kumtolea maneno ya matusi siku moja baada ya kuapishwa kwenye maandamano ya wamawake waliokuwa wakimpinga rais TRUMP.

 

Siku hiyo ya pili TIFFANY alifika katika maonesho hayo akiwa na rafiki zake akiwemo mwanamitindo wa kiume na kukaa nao karibu.

 

LEAH MUSHI

FEBRUARI 15, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI