UN yatafuta suluhu mgogoro eneo la ziwa CHAD
Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameanza safari ya kuzitembelea nchi NNE za eneo la Ziwa CHAD.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameanza safari ya kuzitembelea nchi NNE za eneo la Ziwa CHAD.

 

Lengo la safari hiyo limetajwa kuwa ni kuchunguza mgogoro wa eneo la Ziwa CHAD.

 

Habari zinasema mashambulizi ya Kundi la Boko Haram yamevuruga maisha ya raia katika nchi za eneo la Ziwa Chad.

 

Katika kipindi cha Miaka SABA iliyopita mashambulizi ya kundi hilo yameua maelfu ya watu wasio na hatia na kulazimisha wengine zaidi ya Milioni MBILI kuwa wakimbizi.

 

NIGERIA ndiyo iliyoathiriwa zaidi ambapo raia wengi wa nchi hiyo hasa katika maeneo ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki wamekimbia makazi na nyumba zao na kuishi katika hali ngumu.

 

Mashambulizi hayo pia yamewalazimisha maelfu ya raia kukimbilia katika nchi jirani au maeneo mengine yenye usalama na amani.

 

Idadi kubwa ya raia hao sasa wanaishi katika kambi za wakimbizi wakisumbuliwa na uhaba wa chakula na huduma za afya.

 

Hali hiyo mbaya ya wakimbizi inashuhudiwa pia katika nchi za NIGER, CAMEROON na CHAD. 

 

Sambamba na safari ya ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika nchi za eneo la Ziwa Chad, Jumuiya na Mashirika ya Kimataifa ya Misaada ya Kibinadamu yametahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea maafa makubwa katika eneo hilo.

 

 

GHANIA JUMBE

MACHI 06, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI