Ukame chanzo kikubwa cha hali mbaya ya chakula Afrika
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa –FAO- limesema ukame na vita ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo na hali mbaya ya chakula katika baadhi ya nchi za Afrika hususan nchi zilizoko mashariki mwa bara hilo.
Kilmo kinaathiriwa sana na ukame, Afrika

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa –FAO- limesema ukame na vita ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo na hali mbaya ya chakula katika baadhi ya nchi za Afrika hususan nchi zilizoko mashariki mwa bara hilo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa  FAO, Kostas Stamoulis amesema nchi 37 duniani zikiwemo 28 za Afrika, zinahitaji msaada wa dharura wa chakula kutoka nje. 

Stamoulis amesema licha ya msaada wa chakula kupelekwa katika maeneo kadha duniani bado hakiwafiki walengwa kutokana na vita vinavyoendelea kwenye maeneo hayo.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema baa la njaa limeenea katika nchi kadha za Afrika na Yemen na kuongeza kuwa  hali ya Sudan Kusini ni mbaya

MARTHA NGWIRA

MACHI 3, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI