Zimbabwe yaomba msaada kusaidia walioathirika na mafuriko
Zaidi ya watu 246 wamekufa na wengine elfu mbili kubaki bila ya makazi kutokana na mafuriko tangu mwezi Desemba mwaka jana nchini Zimbabwe.
Waathirika wa mafuriko nchini Zimbabwe wakipokea msaada.

Zaidi ya watu 246 wamekufa na wengine elfu mbili kubaki bila ya makazi kutokana na mafuriko tangu mwezi Desemba mwaka jana nchini Zimbabwe.

         

Zimbabwe imeomba wafadhili wa kimataifa dola za kimarekani milioni mia moja ili kusaidia waliokumbwa na mafuriko hayo.

         

Habari zinasema mafuriko hayo yameathiri zaidi Kusini mwa Zimbabwe ambapo watu wamehamishwa kwa ndege kupelekwa kwenye maeneo salama.

         

Waziri wa Usafiri nchini humo Joram Gumbo amesema madaraja matano katika barabara kuu yamesombwa na maji huku miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ikiharibiwa na mvua hizo.

 

 

DOROTHY MMARI

MACHI 3, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI