Wapiganaji wa M23 wauwawa nchini KONGO-DRC
Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasi ya KONGO – DRC- limesema limewaua wapigaji 23 wa kikundi cha waasi cha M23 ambapo pia limepoteza askari wake wawili wakati ya mapigano yaliyozuka mwishoni mwa Januari mwaka huu.
Kiongozi wa operesheni ya kupambana na waasi wa M23, Kivu kaskazini, Jenerali Leon Mushale

Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasi ya KONGO – DRC- limesema limewaua wapigaji 23 wa kikundi cha waasi cha M23 ambapo pia limepoteza askari wake wawili wakati ya mapigano yaliyozuka mwishoni mwa Januari mwaka huu.

Kiongozi wa operesheni ya kupambana na waasi hao katika Jimbo la Kivu kaskazini, Jenerali  Leon Mushale amewaambia waandishi wa habari kuwa waasi 25 wamejisalimisha na wengine sita wamejeruhiwa katika mji wa Goma

Mapigano hayo yametokea mashariki mwa DRC karibu na mpaka wa nchi hiyo na Uganda Januari  31 na pia kuanzia Februari 20 hadi 22 mwaka huu.

Jenerali Mushale amesema baadhi ya waasi hao wamekimbilia UGANDA na wengine RWANDA kuomba hifadhi.

MARTHA NGWIRA

MACHI 2, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI