Mashindano ya Gofu yafunguliwa
Mkuu wa majeshi mstaafu DAVIS MWAMNYANGE amefungua mashindano ya gofu yaliyoandaliwa kwa ajili ya kusherehekea miaka kumi tangu kutengenezwa uwanja huo wa GOFU LUGALO uliopo Jijini DSM.
GOFU

Mkuu wa majeshi mstaafu DAVIS MWAMNYANGE amefungua mashindano ya gofu yaliyoandaliwa kwa ajili ya kusherehekea miaka kumi tangu kutengenezwa uwanja huo wa GOFU LUGALO uliopo Jijini DSM.

Mashindano hayo yanashirikisha wachezaji kutoka  ndani na nje ya TANZANIA kwa wachezaji  kulipwa na riadhaa .

Mkuu wa majeshi mstaafu DAVIS MWAMNYANGE amesema uwanja wa GOFU , LUGALO haukutengenezwa kwa ajili ya wanajeshi pekee bali ni kwa watu wote ili wajifunze mchezo huo.

Pia amempongeza mwasisi wa uwanja wa GOFU LUGALO mkuu wa majeshi mstaafu GOERGE WAITARA kwa kuthamini mchezo wa GOFU

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ENDIMUND MDORWA akiwakumbusha wachezaji kuzingatia sheria.

Mashindano hayo yanatarajia kufungwa jumapili na RAIS MSTAAFU wa awamu ya nne JAKAYA KIKWETE.

JANE JOHN

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI