MFANYABISHARA KARIAKOO ANASWA NA CD FEKI
Mfanyabiashara Maarufu wa Hoteli hapa nchini ambaye pia anamiliki Hoteli ya BUTTERFLY, KARIAKOO jijini DSM , PHILI ULAYA anashikiliwa na POLISI kwa tuhuma za kuendesha biashara ya uuzaji na usambazaji wa CD za filamu bila ya kufuata utaratibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE akikagua CD katika moja ya duka la kuuzia CD Kariakoo kubaini CD zinazouzwa kinyume na utaratibu.

Mfanyabiashara Maarufu wa Mahoteli hapa nchini ambaye pia anamiliki Hoteli  ya BUTTERFLY  iliyoko KARIAKOO  jijini DSM , PHILI  ULAYA  anashikiliwa na JESHI LA POLISI kwa tuhuma za kuendesha biashara  ya uuzaji na usambazaji wa  CD  za filamu bila ya kufuata utaratibu wa kisheria kutoka kwa mamlaka husika.

 

Mfanyabiashara huyo alikamatwa baada ya kufanyika msako katika eneo la hoteli yake ikiongozwa na Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE kwa ushirikiano na taasisi TANO za serikali  zenye kutoa ithibati ya ufanyaji wa biashara.

 

WAZIRI NAPE anatoa msisitizo wa serikali juu ya kupambana na wafanyabishara ambao hawafuati sheria na kueleza kuwa mkono wa sheria utawafikia hivyo ni lazima wafuate sheria.

 

Pia mesisitiza serikali itaendelea kupambana na wauzaji na wasambazaji wa FILMU ambazo hazifuati maadili ya watanzania kauli ambayo imeungwa mkono na wasimamizi wa biashara ya kazi za filamu nchini.

 

Operesheni hiyo imeelezwa kuwa ni endelevu na awamu itakayofuta itakuwa ni kuwasaka wazalishaji wa FILAMU ambazo zinakiuka taratibu za kisheria zinaongoza tasnia hiyo hapa nchini.

 

 

KULTHUM ALLY

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI