TRUMP kupitia upya amri ya kuwaondoa wahamiaji
Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI amesema atapitia upya uamuzi wake wa kuwaondoa baadhi ya wahamiaji nchini humo.
Rais wa MAREKANI, DONALD TRUMP

Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI amesema atapitia upya uamuzi wake wa kuwaondoa baadhi ya wahamiaji nchini humo.

 

Hatua hiyo imekuja baada Maduka ya biashara kufungwa na wanafunzi kuacha kwenda shule katika mji mbalimbali nchini MAREKANI baada ya maelefu ya waandamanaji kujitokeza kwenye mitaa ya nchi hiyo jana kupinga sera ya rais DONALD TRUMP kuhusu wahamiaji.

 

Wanaharakati wameita siku ya jana kuwa MAREKNI bila wahamiaji ili kuonesha umuhimu wa wahamiaji ambao wanafikia zaidi ya Milioni 40.

 

Kampeni ya rais TRUMP dhidi ya wahamiaji wasio na vibali milioni 12 imempa hofu ya kutokea vitendo vya ugaidi.

 

Baada ya kuapishwa kushika madaraka januari mwaka huu rais TRUMP ametia saini hati ya kuzuia watu kutoka nchini SABA za kiislamu kuingia nchini MAREKANI pamoja na wakimbizi.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI