Mrithi wa kampuni ya SAMSUNG akamatwa
Mrithi wa kampuni ya vifaa vya elektroniki KOREA KUSINI SAMSUNG, LEE JAE-YONG, amekamatwa na vyombo vya usalama ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu kesi ya kuondolewa madarakani rais wa nchi hiyo PARK GUEN-HYE.
LEE JAE-YONG

Viongozi wa mashtaka wanasema kuna uwezekano wa kushikiliwa kwa hadi siku 20 kabla ya maamuzi ya kufungulia rasmi mashtaka.

Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka amesema  LEE alilipa zaidi ya dola  Milioni 35 za Ki- Marekani kwa kampuni  zinazoungwa mkono na CHOI SOON-SIL, rafiki wa Rais PARK  ili kukubali kuunganisha kampuni mbili zilizohusishwa na SAMSUNG.

LEE amekanusha tuhuma hizo.

Kashfa hiyo inatishia kumtoa madarakani PARK ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi kwa muda na Mahakama ya Juu wakati ikichunguza tuhuma dhidi yake.

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI