Waliofariki katika shambulio la bomu PAKISTAN wafikia 72
Idadi ya watu waliokufa kwenye shambulio la kujitoa muhanga katika nyumba ya ibada nchini PAKISTAN imeongezeka na kufikia watu SABINI na WAWILI.
Majeruhi wa Bomu la kujitoa mhanga nchini PAKISTAN akisaidiwa ili kuokoa maisha yake.

Idadi ya watu waliokufa kwenye shambulio la kujitoa muhanga katika nyumba ya ibada nchini PAKISTAN imeongezeka na kufikia watu SABINI na WAWILI.

 

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika katikati mwa waumini katika madhabahu kwenye mji wa SEHWAN, mkoa wa SINDH.

 

Madhabahu hayo ni miongoni mwa yale ya kale zaidi na yanayotukuzwa na yalikuwa yamejaa watu jana Alhamisi, siku hiyo ikichukuliwa kuwa tukufu  kwa waislamu kufanya sala katika madhabahu hayo.

 

Wapiganaji wa ISLAMIC STATE wa TALIBAN nchini PAKISTAN na makundi mengine ya wanamgambo, wamekiri kuhusika na shambulio hilo.

 

Waziri mkuu wa PAKISTAN, NAWAZ SHARIF amelaani shambulio hilo.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI