Mkutano wa usalama waanza mjini MUNICH
Viongozi wa dunia, wanadiplomasia na maafisa wa ulinzi wameanza mkutano mjini MUNICH, UJERUMANI kujadili masuala ya usalama.
Mkutano wa kujadili usalama unaaofanyika mjini MUNICH, UJERUMANI

Viongozi wa dunia, wanadiplomasia na maafisa wa ulinzi wameanza mkutano mjini MUNICH, UJERUMANI kujadili masuala ya usalama.

 

Ujumbe wa MAREKANI katika mkutano huo umewakilishwa na Makamu wa rais  MIKE PENCE, waziri wa ulinzi JIM MATTIS na waziri wa mambo ya ndani JOHN KELLY.

 

Kansela wa UJERUMANI ANGELA MERKEL, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, ANTONIO GUTERRES, rais wa Baraza la Ulaya DONALD TUSK na katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO JENS STOLTENBERG ni miongoni mwa viongozi 30 wa nchi na serikali.

 

Pia mawaziri 80 wa mambo ya nchi za nje na wa ulinzi pamoja na maafisa wengine wanahudhuria mkutano wa MUNICH ulioanza leo.

 

Wajumbe wa UJERUMANI, URUSI, UKRAINE na UFARANSA wanatarajiwa kukutana kando ya mkutano huo kuujadili mgogoro wa mashariki mwa UKRAINE.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI