PAKISTAN waanzisha operesheni ya Usalama
PAKISTAN imeanzisha operesheni ya usalama nchi nzima baada ya bomu kulipuka katika eneo takatifu la SUFI na kuwaua watu 72 wakiwemo watoto 20.
Waziri Mkuu wa PAKISTAN, NAWAZ SHARIF

PAKISTAN imeanzisha operesheni ya usalama nchi nzima baada ya bomu kulipuka katika eneo takatifu la SUFI na kuwaua watu 72 wakiwemo watoto 20.

 

Shambulio hilo linalodaiwa kufanywa na ISLAMIC STATE katika mji wa SENWAH mkoani SINDH limejeruhi zaidi ya watu 250.

 

Polisi wanasema magaidi 18 wameuawa katika operesheni zilizofanywa katika mkoa wa SINDH usiku wa kuamkia leo, huku polisi katika mji wa PESHAWAR wakisema magaidi wengine SABA wameuawa katika eneo la Kaskazini Mashariki.

 

Waziri Mkuu wa PAKISTAN, NAWAZ SHARIF amelilaani shambulio hilo akisema linavuruga juhudi za maendeleo na mshikamano na kuapa kufanya kila awezalo kuilinda nchi yake.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI