HARWARD akataa uteuzi wa Rais DONALD TRUMP
Aliyeteuliwa na Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI kuwa mshauri wa usalama wa taifa baada ya kujiuzulu kwa MICHAEL FLYNN ameukataa uteuzi huo.
ROBERT HARWARD

Aliyeteuliwa na Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI kuwa mshauri wa usalama wa taifa baada ya kujiuzulu kwa MICHAEL FLYNN  ameukataa uteuzi huo.

 

Afisa wa zamani wa jeshi, ROBERT HARWARD ametoa sababu ya kukataa wadhifa huo kuwa,  angependa kupata muda wa kupumzika baada ya kutumikia jeshi la MAREKANI kwa miaka 40

 

Rais TRUMP awali alimteuwa MICHAEL FLYNN kushika nafasi hiyo ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kukutwa na tuhuma za kumdanganya makamu wa rais wa MAREKANI,  MIKE PENCE kuhusu mazungumzo kati yake na balozi wa RUSSIA nchini humo.

 

Awali ANDREW PUZDER mfanyibiashara wa migahawa aliyeteuliwa na rais TRUMP kuwa waziri wa kazi aliondoa jina lake siku moja kabla ya kikao cha SENET kilichojitayarisha kumhoji kuhusu uwezo wake wa kushika nafasi hiyo.

 

Wakati huo huo rais TRUMP amevilaumu baadhi ya vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa kuviita kuwa haviaminiki.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI