TUNISIA yaongeza muda wa hali ya hatari
Serikali ya TUNISIA imeongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu mingine kuanzia Februari 16 mwaka huu.
Rais BEJI CAID ESSEBSI wa TUNISIA

Serikali ya TUNISIA imeongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu mingine  kuanzia Februari 16 mwaka huu.

 

Rais BEJI CAID ESSEBSI  ametangaza hatua hiyo baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, YOUSSEF CHAHED na Spika wa Bunge la nchi hiyo  MOHAMED ENNACEUR.

 

Awali Waziri Mkuu wa nchi hiyo alitangaza kuondolewa hali hiyo ya hatari.

 

Hali ya hatari nchini Tunisia ilianza kutekelezwa  Novemba 24 mwaka 2015 baada ya shambulio la kigaidi dhidi ya basi la askari wa kikosi cha ulinzi cha rais katika mji mkuu wa nchi hiyo TUNIS.

 

Katika shambulio hilo askari 12 waliuawa na wengine kadha kujeruhiwa ambapo  kundi la kigaidi la Daesh lilitangaza kuhusika na shambulio hilo .

 

 

MARTHA NGWIRA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI