Watu zaidi ya elfu Mbili watoweka SUDAN KUSINI
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi kuhusu taarifa za kutoweka watu elfu-20 katika nchi ya SUDAN Kusini.
Mkuu wa kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa Sudan Kusini- UNMISS, DAVID SHEARER

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi kuhusu taarifa za kutoweka watu elfu-20 katika nchi ya SUDAN Kusini.

 

Mkuu wa kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa Sudan Kusini- UNMISS- DAVID SHEARER amesema kukosekana taarifa za kutosha za kutoweka kwa watu hao ni tatizo kubwa kwa serikali ya nchi hiyo pamoja na askari wa  umoja huo.

 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema jitihada mbalimbali zinazofanywa na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa za kuwatafuta watu hao katika jimbo la Upper Nile kaskazini mashariki mwa SUDAN Kusini zimekuwa zikikwamishwa na makundi ya waasi .

 

 

MARTHA NGWIRA

FEBRUARI 17, 2017

 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI