Rais MAGUFULI akutana na viongozi mbalimbali IKULU
Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amekutana na makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya AFRIKA –AfDB-anayeshughulikia masuala ya nishati AMADOU HOTT Ikulu jijini DSM.

Rais Dkt. JOHN MAGUFULI  amekutana na makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya AFRIKA –AfDB-anayeshughulikia masuala ya nishati AMADOU HOTT  Ikulu jijini DSM.

 

Wakati wa mazungumzo yao HOTT ameelezea  kuguswa na dhamira ya Rais MAGUFULI ya kuongeza uzalishaji wa umeme wa gharama mnafuu kwa ajili ya kufanikisha  mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda.

 

Kwa upande wake Rais MAGUFULI amesema TANZANIA iko tayari  kutoa ushirikiano wakati wowote utakapohitajika kufanya hivyo ili kuhakikisha dhamira hiyo inafanikiwa.

 

Wakati huo huo Rais MAGUFULI amekutana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterprises inayomiliki kampuni ya simu ya Airtel Duniani, SUNIL BHARTI MITTAL na kuzungumzia utendaji wa kampuni hiyo nchini.

 

SUNIL BHARTI MITTAL amesema yuko tayari kuingiza kampuni ya Airtel Tanzania katika soko la hisa la Dar es Salaam ili Watanzania wapate fursa ya kumiliki kampuni hiyo kwa kununua hisa.

 

Aidha Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchini JEAN PIERRE TSHAMPANGA MUTAMBA Ikulu  jijini Dar es Salaam.

 

 

TAARIFA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI