Bilioni 3 zatengwa kutekeleza miradi ya maji
Serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoani TANGA katika mwaka wa fedha wa 2016/17 ili kuhakikisha watu wanapata maji safi na salama hususan maeneo ya vijijini.
Naibu waziri wa Wizara ya Maji Mhandisi, ISSAC KAMWELWE

Serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya utekelezaji wa  miradi ya maji mkoani TANGA katika mwaka wa fedha wa 2016/17 ili kuhakikisha watu wanapata maji safi na salama hususan maeneo ya vijijini.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Wizara ya Maji Mhandisi ISSAC KAMWELWE wakati akizungumza na Wataalam wa maji na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya LUSHOTO.

Mhandisi ISSAC KAMWELWE yupo wilayani LUSHOTO kwa ziara ya siku mbili kwa lengo la kukagua upatikanaji wa huduma ya majisafi miradi ya maji.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya LUSHOTO,  JANUARY RUGANGIKA amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kufanya tathmini ya miradi ya maji ili kujua namna fedha zinavyotumika.

JOACHIM KAPEMBE

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI