Wakazi wa MASASI watakiwa kulinda vyanzo vya maji
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya MASASI mkoani MTWARA limewataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji zinazochangia katika uharibifu wa mazingira
Halmashauri ya mji wa MASASI

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya MASASI mkoani MTWARA limewataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji zinazochangia katika uharibifu wa mazingira.

 

Baraza hilo limesema bila ya kuacha kufanya hivyo vyanzo vya maji vitaathirika na kuleta madhara kwa kizazi cha sasa na baadae.

 

Baraza hilo limesema licha ya wakazi wa wilaya hiyo kupewa elimu ya utunzaji wa mazingira bado wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu kama kilimo katika vyanzo vya maji  na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa maji katika vyanzo hivyo.

 

Kwa upande wake Afisa Mazingira katika halmashauri hiyo KULWA MAHIGE  amekiri kuwepo kwa changamoto na kusema ofisi yake inaendelea kuelimisha jamii juu ya faida za kutunza nakulinda mazingira.

 

 

MARTINA NGULUMBI

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI