Halmashauri za UNGUJA zatakiwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa pili wa Rais
Watumishi wa Halmashauri na Wilaya zote mjini Unguja wametakiwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ZANZIBAR katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo kwa wananchi.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd

Watumishi wa Halmashauri na Wilaya zote mjini Unguja wametakiwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ZANZIBAR katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza kasi  ya ukuaji  wa maendeleo kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais HAMADI KASSIM HAJI wakati wa mafunzo kwa watumishi juu ya namna ya kutumia fedha za miradi ya maendeleo ambapo amesema serikali imewapa watumishi hao jukumu la kuwaongoza wananchi katika majimbo yao na kuwaletea maendeleo.

Naibu Katibu mkuu HAMAD KASSIM HAJI amesema watendaji wa halmashari na majimbo hawana budi kushirikiana katika kubuni miradi ili kuharakisha maendeleo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya uratibu wa shughuli za serikali ofisi ya makamu   wa pili wa rais KHALID BAKARI AMRAN amewatahadharisha watumishi hao kuwa serikali haita muonea haya mtumishi yeyote atakaye tumia vibaya fedha za serikali.

SWAUMU MAVURA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI