MWAUWASA yasaini mkataba wa ujenzi wa miradi ya maji safi
Serikali kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira utakaosaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika jiji hilo na mikoa ya jirani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi GERSON LWENGE akizungumza wakati wa hafla ya utiliwaji saini ya mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira utakaosaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika jiji hilo na mikoa ya jirani.

Serikali  kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza  (MWAUWASA) imesaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira utakaosaidia upatikanaji wa  huduma ya maji katika jiji hilo na mikoa ya jirani.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiliwaji saini ya mikataba hiyo ,Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi GERSON LWENGE amewaagiza wakandarasi waliopewa zabuni ya ujenzi wa miradi hiyo, itakayogharimu billion 245  kuzingatia ubora wa kazi na  muda ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Miradi hiyo ambayo inafadhiliwa na serikali kwa kushirikiana na  Benki ya uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD)  itakamilika mwaka 2019 na inatarajiwa kuwanufaisha Zaidi ya wakazi laki moja wanaoishi katika katika miji ya Mwanza, Lamadi, Magu, Misungwi, Musoma na Bukoba.

AMICUS BUTUNGA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI