Rais Magufuli ataka wananchi kufanya kazi kwa bidii
Rais John Magufuli ametoa wito kwa wananchi kupuuza baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la njaa na badala yake wajikite kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeo ya taifa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Anthony Mtaka wakifurahia jambo. Rais Magufuli yupo kwenye ziara mkoani Simiyu

Rais John Magufuli ametoa wito kwa wananchi kupuuza baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotoa taarifa kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la njaa na badala yake wajikite kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeo ya taifa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu Rais Magufuli amesema taarifa hizo ni uzushi usiotakia mema nchi kwani akiwa ni Rais wa Tanzania ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za njaa kwa mujibu wa sheria taratibu za nchi.

Rais Magufuli ambaye yuko ziarani mkoani Simiyu pamoja na mambo mengine amezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu nwa kilometa 71.2 kutoka Lamadi hadi Bariadi huku barabara hiyo ikitajwa kuwa na faida lukuki.

GREYSON KAKURU

JANUARI 11,  2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI