Wazanzibar washauriwa kumuenzi Karume
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakazi wa Zanzibar kumuenzi kwa vitendo muasisi wa Mapinduzi hayo Hayati Abeid Amani Karume kwa kuboresha makazi Visiwani humo.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi Mbweni.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakazi wa Zanzibar kumuenzi kwa vitendo muasisi wa Mapinduzi hayo Hayati Abeid Amani Karume kwa kuboresha makazi Visiwani humo.

 

Makamu wa Rais ametoa wito huo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi Mbweni na kuongeza kuwa wakati wa uhai wake Mzee Karume alihakikisha kunakuwepo makazi bora kwa kujenga nyumba za kisasa mara baada ya mapinduzi.

 

Mradi wa ujenzi wa nyumba za makaazi unajengwa na mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar – ZSSF.

 

Makamu wa Rais ameutaka mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar kutumia fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania Bara ili kukuza mapato ya mfuko huo.

 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF, Abdulwakil Haji Hafidh amesema mradi huo utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwemo za maduka, kumbi za kisasa za mikutano na michezo ya watoto.

 

Awamu ya kwanza ya mradi wa nyumba za makaazi unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.

 

 

RUKIA MPUTILA

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI