Washauriwa kujitokeza kuadhimisha mapinduzi
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mohmoud ametoa wito kwa wakazi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kusherekea sherehe za mapinduzi zitakazofanyika katika uwanja wa Amani.
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mohmoud

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mohmoud ametoa wito kwa wakazi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kusherekea sherehe za mapinduzi zitakazofanyika katika uwanja wa Amani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Mohmoud amesema mgeni rasmi katika maadhimishi hayo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

 

Akizungumzia kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mohmoud amesema viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara na visiwani watashiriki na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi.

 

Kwa upande wake Kamishna wa jeshi la polisi HAMDAM OMAR MAKAME amesema vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na  jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mkoa ili kuhakikisha amani na utulivu inaendeleo kuwepo katika kipindi cha kabla na baada ya sherehe za mapinduzi

 

Kamishna MAKAME ameongeza kuwa jeshi la polisi litaimarisha ulinzi na usalama katika usiku wa mkesha wa kuamkia siku ya mapindizi.

 

 

SWAUMU MAVURA

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI