Manchester United kumuuza Morgan Schneiderlin
Manchester United imekubali kumuuza kiungo wa kati Morgan Schneiderlin kwa pauni Milioni 22 tayari kuitumikia timu ya Everton.
Morgan Schneiderlin

Manchester United imekubali kumuuza kiungo wa kati Morgan Schneiderlin kwa pauni Milioni 22 tayari kuitumikia timu ya Everton.

 

Mfaransa huyo, alinunuliwa na Manchester United kwa kitita cha pauni Milioni 25 kutoka Southampton mwezi Julai mwaka 2015 chini ya ukufunzi wa Louis van Gaal.

 

Ameiwakilisha Man U mara 47, japo chini ya ukufunzi wa Jose Morinho msimu amecheza mara 8 pekee, mara tatu katika dimba la ligi kuu ya Uingereza.

 

Hayo yakiarifiwa, mshambuliaji Oumar Niasse wa Everton atahama kwa mkopo kuelekea Hull City japo makubaliano ya kibinafsi bado hayajaafikiwa.

 

Raia huyo wa Senegal alijiunga na Everton mwezi Februari mwaka 2016 kwa kitita cha pauni milioni 13.5 kutoka Lokomotiv Moscow japo amechezea klabu hiyo mara saba pekee.

 

 

JANE JOHN

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI