Rais MAGUFULI awashauri wakulima kulima mazao yanayostahimili ukame
Rais DKT JOHN MAGUFULI amezungumzia umuhimu wa wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili waweze kukabiliana na uhaba wa chakula unaoweza kutokea kutokana na mvua za masika kuchelewa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Rais, DKT JOHN MAGUFULI.

Rais DKT  JOHN MAGUFULI amezungumzia umuhimu wa wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili waweze kukabiliana na uhaba wa chakula unaoweza kutokea kutokana na mvua za masika  kuchelewa  kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha MASANZAKONA wilaya ya BUSEGA mkoani SIMIYU kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo, Rais MAGUFULI amesema mazao kama mtama na uwele yanastahimili ukame hivyo ni vyema yakalimwa ili kukabilian na uhaba wa mvua katika baadhi ya maeneo nchini.

Rais MAGUFULI pia ameahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la maji la muda mrefu linalowakabili wakazi wa wilaya ya BUSEGA mkoani Simiyu.

Akiwa mkoani SIMIYU atatembelea wilaya za BARIADI na MASWA na baadae kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika wilaya hizo.

TAARIFA

JANUARI 11,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI