Halmashauri ya Mji KASULU imetoa vitambulisho 1,800 kwa ajili ya huduma ya afya kwa wazee
Baadhi ya wazee wa wilaya ya KASULU mkoani KIGOMA wameiomba serikali kupitia halmashauri zake kupanga bajeti kwa ajili ya huduma za wazee na kuongeza kasi ya utoaji vitambulisho vya huduma za afya kwa wazee.
Wazee, Tanzania. Wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, wazee kama hawa wameiomba Serikali serikali kupitia halmashauri zake kupanga bajeti kwa ajili ya huduma za wazee.

Baadhi ya wazee wa wilaya ya KASULU mkoani KIGOMA wameiomba serikali  kupitia halmashauri zake kupanga bajeti kwa ajili ya  huduma za wazee na kuongeza kasi ya utoaji vitambulisho vya  huduma za afya kwa wazee.

 

Wakizungumza katika mahojiano maalum na TBC wamesema kuwa jamii  na serikali kwa ujumla inapaswa kuendelea kuwathamini, kuwasaidia na kuenzi wazee kwa kuwa wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa katika nyanja mbalimbali zikiwemo za ulinzi na uzalishaji mali hasa wakati wa ujana wao.

 

 

Kwa upande wake  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji KASULU, DASTAN MSHANA amesema kuwa  utambuzi na utoaji  vitambulisho kwa wazee ni kazi  endelevu ambayo itakuwa ikifanyika kadri fedha zinapopatikana.

 

Katika jitihada za kuboresha huduma za tiba  kwa wazee Halmashauri ya Mji  Kasulu imetoa vitambulisho 1,800 kwa wazee kutoka kata 8 kati ya 15 zilizopo katika Halmashauri hiyo.

 

 

EDWARD KONDELA

JANUARI 11,2017 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI