Walimu 765 wa chekechea wapewa mafunzo kamilishi
Walimu 765 wa elimu ya awali kutoka shule zote za Halmashauri za mkoa wa RUVUMA wanapatiwa mafunzo kamilishi baada ya Taasisi ya Elimu Tanzania kuboresha mtaala wa elimu ya mafunzo ya awali.
Picha kutoka Maktaba. Wanafunzi wa Chekechea na Walimu wao.

Walimu 765 wa elimu ya awali kutoka shule zote za Halmashauri za mkoa wa RUVUMA wanapatiwa mafunzo kamilishi baada ya Taasisi ya Elimu Tanzania kuboresha mtaala wa elimu ya mafunzo ya awali.

Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Taasisi hiyo, FREDRICK MKEBESI amesema mafunzo hayo yanatolewa ili kuwajengea uwezo walimu wa  elimu ya awali yatakayowawezesha wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Afisa Elimu wa mkoa wa RUVUMA, GHARAMA KINDERU amesema ni muhimu walimu wakafuatilia vYema mafunzo hayo  ili waweze kuwaelimisha walimu wenzao waTAkaporudi shuleni.

Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa mkoa wa RUVUMA, HASSAN BENDEYEKO amesema mafunzo hayo yanatolewa nchi nzima ili kuwezesha watoto wote wa elimu ya awali kupata elimu stahiki.

NOELA NJAWA

JANUARI 11,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI