Wajasiriamali wadai VIKOBA si endelevu
Wajasirimali wadogo ambao ni wanachama wa vyama vya akiba na mikopo ( VIKOBA) katika wilaya ya Iringa wamesema kuwa vyama hivyo si endelevu kwa vile wanachama wake hawana elimu ya kuendesha vyama hivyo.
Sanduku la kuwekea fedha na nyaraka muhimu za ViIKOBA

Wajasirimali wadogo ambao ni wanachama wa vyama vya akiba na mikopo ( VIKOBA) katika wilaya ya Iringa wamesema kuwa vyama hivyo si  endelevu kwa vile wanachama wake hawana elimu ya kuendesha vyama hivyo.

Wakizungumza kwenye mafunzo ya VIKOBA endelevu wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha TUHEGELYE wamesema kuwa kutokana na uelewa mdogo, vyama hivyo vimekuwa vikikabiliwa na  migogoro ya uongozi.
 
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya VIKOBA kitaifa Aidan Kumburu amesema ni lazima kuwepo na malengo wakati wa kukopa fedha, ili vyama hivyo viwe endelevu.

Akisoma taarifa ya fedha ya kikundi hicho, Mweka hazina TULABESA MERERE amesema wanachama wake wameweza kufungua miradi mbalimbali na wana mpango wa kununua ekari 50 kwa ajili ya kilimo.
 
IRENE MWAKALINGA

JANUARI 11,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI