Wadudu waendelea kutishia zao la pamba MWANZA
Wakulima wa zao la pamba wilayani KWIMBA mkoani MWANZA wameiomba serikali kuwapatia dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo.
Zao la PAMBA

Wakulima wa  zao la pamba wilayani KWIMBA mkoani MWANZA wameiomba serikali kuwapatia dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo.

 

Baadhi ya wakulima wa zao hilo kutoka vijiji vya kilyaboya, Manawa na solwe wamemweleza mkuu wa mkoa mwanza JOHN MONGELA kuwa  hadi sasa hawajapata dawa hizo huku mashamba yao yakishambuliwa na  wadudu hao.

 

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa MWANZA, JOHN MONGELLA akatoa maelekezo kwa kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza pembejeo za kilimo wilayani KWIMBA ya ICK kuhakikisha dawa hiyo inawafikia wakulima la sivyo serikali itaichukulia hatua za kisheria.

 

 

Hali hiyo inajitokeza takribani miezi mitatu tangu kuanza kwa msimu wa kilimo cha zao la pamba nchini, ambacho serikali inawekqa jitihaza za kufufua zao hilo kibiashara.

 

 

AMICUS BUTUNGA

JANUARI 11,2017

 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI