Wafanyabiashara soko la MBAGALA ZAKHEM walalamikia miundo mbinu mibovu.
Wafanyabiashara wa soko la mbagala zakhem manispaa ya temeke jijini DAR ES SALAAM wamelalamikia kufanya biashara katika mazingira magumu kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu sokoni hapo.

Wafanyabiashara wa soko la mbagala zakhem manispaa ya temeke jijini DAR ES SALAAM  wamelalamikia kufanya biashara katika mazingira magumu kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu sokoni hapo.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wameeleza kuwa ubovu wa miundombinu hiyo ni pamoja na vibanda kuwa chakavu na kushindwa kufanya biashara kipindi cha mvua huku wakinamama lishe wakipika vyakula vyao hovyo kutokana na kutokuwepo kwa mpangilio wa soko.

Akizungumzia hali hiyo katibu wa soko hilo la mbagala zakhem JUMA MEMBE ameilaumu manispaa ya temeke kwa kutotoa kibali cha  kujenga soko lingine kwa licha ya kumpata  mwekezaji wa kujengea soko hilo kwa mkopo.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 10, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI