TRUMP kumteua mkwe wake kuwa mshauri mwandamizi ikulu ya WHITE HOUSE
Rais Mtarajiwa wa Marekani DONALD TRUMP anatarajiwa kumteua mkwe wake JARED KUSHNER kama Mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mteule wa Marekani DONALD TRUMP.

Rais Mtarajiwa wa Marekani DONALD TRUMP  anatarajiwa kumteua mkwe wake JARED KUSHNER  kama Mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

 

KUSHNER  mwenye umri wa miaka 25 ambaye amemuoa binti mkubwa wa TRUMP , IVANKA ambaye  alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha TRUMP  kushinda.

 

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

 

Uteuzi huo unatarajiwa kwa kiasi kikubwa, na hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

 

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 10, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI