Nusu fainali kombe la Mapinduzi Jumanne
Nusu fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi inatarajia kupigwa Jumanne wiki hii katika uwanja wa AMANI VISIWANI ZANZIBAR kwa michezo miwili.
Wachezaji wa AZAM kabla ya mechi dhidi ya YANGA katika kombe la Mapinduzi

Nusu fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi inatarajia kupigwa Jumanne wiki hii katika uwanja wa AMANI VISIWANI ZANZIBAR kwa michezo miwili.

Katika kuelekea michezo hiyo Katibu wa kamati ya mashindano amesema watauza tiketi kulingana na idadi ya uwanja hawataruhusu watu kukaa kwenye TRACK.

Mchezo wa mapema utazikutanisha AZAM FC ambao walimtandika YANGA katika hatua ya makundi magoli MANNE kwa bila dhidi ya TAIFA JANG’OMBE.

Wakati mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki ni mchezo wa watani wa jadi SIMBA na YANGA watakapopepetana saa mbili usiku katika uwanja huo huo wa AMANI.

JANE JOHN

JANUARI 09, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI